Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, Mwenyekiti wa Baraza la Maulamaa wa Kishia wa Pakistan, katika kujibu matamshi ya hivi karibuni ya matusi ya Rais wa Marekani kuhusu Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei (daama dhilluh), ametoa taarifa na kulaani vikali sana lugha hiyo isiyofaa.
Akiwa amesisitiza nafasi ya kipekee na yenye athari ya Ayatollah Khamenei katika ulimwengu wa Kiislamu, amesema: Yeye si tu Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, bali ni shakhsia ya kimataifa anayeheshimiwa na mataifa ya Kiislamu, na ana nafasi maalumu katika Ummah wa Kiislamu, hasa katika jamii ya Kishia. Hivyo basi, kuheshimu adabu na taadhima katika maneno ni kiwango cha chini kabisa kinachotarajiwa kutoka kwa viongozi wa kimataifa.
Mwanazuoni huyu mashuhuri wa Pakistan, huku kuonya kuhusiana na madhara yatokanayo na matamshi kama hayo yasiyo ya busara, amesema: Madola ya kibeberu yanapaswa kuepuka kutoa kauli za kichochezi na zisizo na msingi, kwa kuwa dharau za namna hii zinaweza kuamsha majibu makubwa kutoka kwa marajii, maulamaa na mataifa ya Kiislamu – majibu ambayo huenda yakasababisha athari zisizoweza kurekebishwa.
Akiendelea, alisema: Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, kutokana na misimamo yake ya kishujaa, yenye busara na ya wazi, kwa mara nyingine ameonesha kuwa heshima, uhuru na ghera ya Kiislamu ni misingi isiyowekewa masharti wala mazungumzo ya kufanyiwa biashara. Ayatollah Khamenei, kwa maneno yake ya wazi na thabiti, ameshikilia kikamilifu nafasi halisi ya uongozi wa Ummah wa Kiislamu na anastahili kupongezwa na kuungwa mkono na mataifa ya Kiislamu.
Mwisho, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Naqvi alisisitiza kuwa: Ayatollah Khamenei kwa sasa ni nembo ya umoja, mwamko na heshima ya Ummah wa Kiislamu, na ulimwengu wa Kiislamu unapaswa kuuthamini uongozi huu wa kimungu na wa kuleta nuru. Bila shaka, yeye ni sauti ya pamoja na yenye nguvu ya Waislamu mbele ya mabeberu wa dunia.
Maoni yako